Muungano wa makanisa kadhaa kutoka uliokuwa mkoa wa Kati,Kenya umetangaza mwezi mmoja wa maombi dhidi ya Rais wa Marekani Barack Obama kuhusu msukumo wake wa utambuzi wa mashoga na wasagaji.
Muungano huo kwa jina Central Region Inter-Ministerial Leaders Summit unaojumuisha makanisa ya kipentokoste na yale ya kiasili ulisema kuwa Bw Obama anahitaji mguso wa kiroho ili aelewe kuwa tamaduni za Kiafrika, utawala na dini ni ndugu moja na ambazo haziwezi kutenganishwa.
Walisema kuwa maombi hayo yatajumuisha kuwaombea wale wote ambao wako katika hali hiyo ya kimapenzi ili wabadilike na wajiunge na walio wengi katika kutukuza na kueneza uhusiano kati ya Mume na Mke kama mtazamo wa Mungu kuhusu ndoa.
Aidha, watatakiwa kutenga ibada za kumuomba Mungu asikasirikie binadamu kufuatia hujuma za dini ambazo huzuka wakati binadamu hao wameanza kutumia masomo na maarifa yao visivyo.
Katika ibada iliyoongozwa na mwakilishi wa tawi la mashariki mwa Mlima Kenya la chama hicho, Kasisi Geoffrey Njuguna wa KAG katika kanisa la Ngurubani Jimbo la Kirinyaga, Jumapili, walisema kuwa Afrika na watu wake weusi hawana nafasi ya "kuzorotesha maadili mema kwa misingi ya haki na usawa wa binadamu."
Walikuwa wakijibu hoja kwamba Rais huyo wa Marekani amezomea serikali ya Uganda kufuatia kuidhinishwa kwa sheria na Rais Yoweri Museveni za kukadamiza mashoga na wasagaji.
Walisema kuwa Marekani na mataifa mengine ya Ulaya yako na haki za kujitafutia umaarufu kupitia sheria za kukubali walio katika uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja bora tu wasijaribu kuambukiza Afrika tamaduni hizo "potovu."
Bw Njuguna alisema kuwa Mungu hakuwa hajatafakari hayo yote alipoumba Adamu na Eva na kuwaweka katika bustani la kifahari la Edeni.
"Mungu angekuwa kama Obama, angeumba wanawake wawili au wanaume wawili na kisha awape idhini ya kuoana," akasema.
Alimtaka Bw Obama aelewe kuwa ikiwa urafiki kati ya Waafrika na Wazungu utadumishwa kufuatia kukubalia ushoga na usagaji "basi achukue urafiki huo wake na kisha augawie watu wa Marekani na sio Waafrika."
Laana
Bw Njuguna alinukuu vipengele vya Bibilia vinavyokashifu mapenzi ya jinsia moja huku akiwataka washirika wamnyenyekee Mwenyezi Mungu asije akatoa laana kwa wachungaji kwa kunyamaa wakati maadili mema katika jamii yanalengwa na matapeli wa kuhujumu neno la Mungu.
Hatua hiyo ilijiri huku Wabunge wa Kenya wakiendelea kujadili hoja ya Mbunge wa Kiharu Bw Irungu Kang'ata ya kukemea ushoga na usagaji.
Hata hivyo, waziri wa Afya Bw James Macharia ameonya kuwa mjadala huo unawabagua walio katika hali hiyo na kwa sasa wanahofia kujiweka katika mpango wa madawa ya Ukimwi kwa walioathirika.
Bw Macharia ametaka nchi itulie na itafute njia badala za kujadili suala hilo bila ya kuonyesha chuki kwa walio katika hali hiyo ya mapenzi ya jinsia moja.