Mwanamuziki wa Bongo flava ambaye hivi karibuni alikumbwa na majanga ya utumiaji wa madawa ya kulevya hali iliyompelekea kuugua kwa mda mrefu sana hata kufikia karibu na kupoteza maisha, amefunguka na kukanusha taarifa zilizoripotiwa awali kwamba kwa sasa ameamua kumrudia Mungu na kuokoka baada ya kujiunga na kanisa la Siloam lililopo Dar es Salaam ambapo pia alibatizwa kwa maji mengi kama ilivyo kanuni kwa makanisa yote ya kipentekoste yanayoamini katika ubatizo wa maji mengi.
Aidha mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba sana miaka ya nyuma katika muziki wa bongo flava alijikuta aidhoofika afya yake kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya na kujikuta akiwa katika mazingira hatarishi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa Ray C ambayo blog hii imeyanasa,Ray C ameeleza kwamba anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka na hiki ndicho alichokisema kuhusu Kuokoka.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi
Kuhusu suala la kuokoka, hivi ndivyo alivyosema Ray C
"ukweli ni kwamba mwanzoni nilikua Mkatoliki lakini hivi karibuni nilibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yangu anayesali kwenye kanisa hilo"
“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam. Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu wanatafsiri kuwa nimeokoka"
“Watu wakisikia mtu anasema ameokoka wanatafuta vitu ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka lakini mahubiri yananiweka huru na nakuwa na amani zaidi,” alisema Ray C.