Rais Kikwete aungana maelfu ya wakazi wa Mwanza kumzika Askofu mkuu Dr.Moses Kulola
byAdmin-
0
hatimaye mwili wa askofu mkuu wa kanisa la EAGT na baba wa kiroho wa watumishi wa Mungu mbalimbali nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla Dr.Moses Kulola umezikwa jumatano hii katika kanisa la EAGT Bugando jijini Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano Dr.Jakaya Kikwete akiongozana na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na waziri mkuu aliyejiuzuru na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowasa.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi kumzika Askofu mkuu Dr.Moses Kulola
kwa upande wa vyama vingine vya kisiasa viongozi wa kitaifa waliohudhuria mazishi ya askofu Dr.Moses Kulola ni pamoja na Katibu mkuu wa Chama hicho ndugu Wilbroad Slaa aliyeongozana na wabunge wake mbalimbali.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) Wilbroad Slaa (wa
pili toka kushoto mbele) akiwa na mkewe, huku Mbunge wa Nyamagana
Ezekiel Wenje (kushoto) akionekana .
Katika Salaam zake kwa watanzania kwa kuondokewa na mtu huyu muhimu kwa taifa kiroho na kimwili pia Rais Jakaya alitumia mda wake kumuelezea Askofu Dr.Moses kwa namna alivyomfaham kwa kipindi kirefu sasa na kwa namna walivyofanya nae kazi katika kudumisha amani nchini Tanzania
Bofya hapo usikie alichokisema Rais Kikwete
hali ya simanzi na majonzi ilitawala katika mazishi hayo ambapo pia Rais Kikwete alimuelezea Dr.Moses Kulola kama mtu aliyefahamiana nae mda mrefu na mtu ambaye aliwahi pia kwenda ikulu na kumuombea na pia kuiombea nchi ya Tanzania idumu katika Amani na mshikamano
Aidha Rais Kikwete alimuelezea Dr.Moses Kulola kama mtu ambaye alikua mkweli mpenda watu watu na mtu ambaye hakua na ubaguzi wa kabila,dini rangi wala dhehebu na ndio maana hata leo hii watu wa madhehebu yote wamehudhuria hata katika mazishi yake.
"Mimi sio msukuma wala mimi sio mkristu lakini kikubwa kilichonifanya nifike katika mazishi ya ndugu yetu na mpendwa wetu huyu askofu mkuu Dr.Moses Kulola ni vile maisha yake aliyoishi hapa duniani ambayo ni mahubiri tosha
aliisimamia kweli bila kuogopa wala kutetereka ,,,,,penye baya alisema hili ni baya na penye zuri alisema hili ni zuri....kama asingekua mtu wa namna hiyo wala asingekua rafiki yangu... kuna kipindi alishakuja yeye pamoja na mama mpaka kwangu ikulu akanambia nimekuja nataka nikuombee wewe binafsi na pia niiombee nchi ya Tanzania kupitia wewe Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ufanikiwe na upate kuongoza vema usiogope Mungu yupo pamoja nawe.
kwa namna mtu huyu maisha yake alivyoishi binafsi nimehuzunishwa sana baada ya kusikia kifo chake kwani taifa limepoteza mtu wa muhimu sana mtu aliyekua kila kukicha akiiombea tanzania iwe na amani na mshkamano na ndio maana leo hii wote tupo hapa bila kujali vyama vyetu wanasiasa dini zetu wala kabila zetu....kikubwa tumuenzi kwa kutenda yale aliyotufundisha. alisema Rais Jakaya Kikwete
Picha na matukio yote yaliyojiri katika mazishi ya shujaa wa injili Askofu Dr.Moses Kulola ni kama zinavyoonekana hapa chini
Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika eneo ilipofanyika ibada ya mazishi ya askofu Moses Kulola
Mwalim Christopher Mwakasege
Mh.William Ngeleja akielezea kwa namna alivyoguswa na msiba huu
Mchungaji Msigwa na mbunge wa Iringa akielezea kwa namna alivyomfaham Askofu Moses Kulola
Maaskofu wakishusha sanduku lenye mwili wa askofu Dr.Moses Kulola
mama mjane akiweka udongo kwenye kaburi la mumewe Askofu Moses Kulola
Mke wa Shujaa wa Injili akiweka Shada ya Maua
Mh.Edward Lowasa akiweka shada la Maua juu ya kaburi la Askofu Dr.Moses Kulola
Katibu mkuu wa chama cha Demokrasi na maendeleo CHADEMA akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Dr.Moses Kulola
Mbunge wa Nyamagana Mh.Hezekia Wenje akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Dr.Moses Kulola
Rais Jakaya Kikwete akiosha mikono baada ya kumaliza kuweka udongo kwenye kaburi la Askofu Moses Kulola
makamu askofu Asumwisye Mwaisabila akiongoza Ibada ya mazishi ya askofu Moses Kulola
Add caption
Mwigizaji
wa Ze Komedi ambaye pia ni mwimbaji wa njimbo za Injili Emanuel Mgaya
maarufu kama Masanja Mkandamizaji alitumika kutoa neno kwa njia ya
uimbaji ambapo vilevile aliwagusa wengi na maneno yake.
Mwigizaji
wa Ze Komedi ambaye pia ni mwimbaji wa njimbo za Injili Emanuel Mgaya
maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiwa na vijana wa kundi lake
alitumika kutoa neno kwa njia ya uimbaji.
Mwimbaji maarufu wa Muziki wa Injili Afrika Mashariki Flora Mbasha aliimba wimbo mahsusi pamoja na wajukuu wenzake wa Askofu Moses Kulola.
Maaskofu wa kanda wakishusha mwili wa Askofu Moses Kulola
makamu Askofu mkuu Asumwisye Mwaisabila akiwa na Katibu mkuu wa EAGT Mchungaji Brown Mwakipesile katika kuongoza ibada ya maziko
Dr.Wilbroad slaa katibu mkuu wa CHADEMA akiweka udongo katika kaburi la Askofu Dr.Moses Kulola
Mchungaji Mwizarubi akifunga ibada ya mazishi kwa maombi
Gari
la kwanza kutoka eneo hili lilikuwa la Mhe. Rais JK. ambapo watu wengi
walifurika nje ya lango kuu ambalo lilifungwa kutokana na watu
walioinngia eneo la uwanja kufikia idadi ya usalama.
Waziri
Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa
akitoka eneo la uwanja wa EAGT Ushirika wa Bugando jijini mwanza huku
wananchi wakisalimiana naye.
wanahabari ambao kwa pamoja wamekuletea picha za matukio yote haya yaliyojiri siku hii