Kiongozi wa huduma ya maombezi ya GRC ubungo kibangu Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kama mzee wa upako amelishauri kanisa la Tanzania Assemblies of God kuacha kudai mali zote zinazotumiwa na wafuasi wa aliyekua mwasisi wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God EAGT Askofu Dr.Moses Kulola aliyefariki Agosti 29 mwaka huu na kuzikwa kanisani Bugando jijini Mwanza
Aidha Mzee wa upako ameeleza kwamba ukubwa na mafanikio ya kanisa la TAG yanatokana na huduma ya marehemu Kulola hivyo kuendelea kupambana mahakamani kudai mali walizovumilia kutokua nazo kwa zaidi ya miaka 20 ni sawa na kujitafutia laana.
TAG wagange wajayo waachane kabisa na na jambo hilo,na kuongeza kua maoni yake hayo yanazingatia ukweli kwamba watu wengi hata waumini wa makanisa hayo mawili hawajui mengi juu ya mgogoro huo.
Hata mkuu wan chi Rais Jakaya Kikwete niliongea naye alikua hajui kama kulikua na watu wameshitaki ili kulola asizikwe pale Rais Kikwete alishangaa sana…nawashauri waache” alisisitiza.
Mzee wa upako amesema katika hali ya kiungwana TAG walipaswa kujiuliza wao watapoteza nini ikiwa wataachia makanisa hayo wanayodai ni ya kwao kasha wafikirie adha ambayo itawapata wale ambao tayari wanayatumia kwa kuzingatia kwamba wote wanafanya kazi chini ya Mungu mmoja.
Mzee wa upako amesema kwamba kama ombi la TAG litakubaliwa mahakamani EAGT watatawanyika waanze kuhaha kutafuta pa kuabudia huko TAG wakibaki na majengo wazi ndipo waanze kutafuta watu wa kuyatumia hivyo kiroho kutakua na athari kubwa.
Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kama mzee wa upako |