Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT) linatarajia kuanza mwezi ujao kwa machungu mapya kabisa huku yale ya kuaga dunia kwa aliyekua Askofu wake mkuu Askofu Moses Kulola hayajapoa , Kanisa hilo linatakiwa kusimama mahakamani mwezi ujao Oktoba 1 kujitetea ili waumini wake wasiondolewe kwenye kanisa la Bugando ambako askofu Kulola amezikwa.
Katika shauri hilo lenye nambari 121/2013 iliyofunguliwa mwaka huu haya kabla Askofu Kulola hajafariki ambapo kwa maelezo ya Askofu Mkuu wa TAG Dkt. Barnabas Mtokambali kesi hiyo ya kudai kanisa la Bugando ni mwanzo wa tu katika kudai mengine mengi.
EAGT inatetewa na wakili Deocles Rutahidurwa wa Rwelu Attorney,Mwanza
Kwa mujibu wa nyaraka za TAG makanisa mengine yaliyoko kwenye orodha inayotakiwa EAGT wayaachie ni pamoja na yale yaliyopo Tabora, Dar es Salaam,Mbeya,Arusha ,Shinyanga,Tanga,Mwanza,Morogoro,Pwani,Singida,Kilimanjaro, na maeneo mengine nchini.
Kwa Dar es Salaam makanisa yanayotakiwa na TAG ni pamoja na kanisa la Temeke ambako mwili wa wa marehemu Kulola uliagwa kwa mara ya kwanza kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza.
akielezea namna ambavyo kanisa la EAGT wamejiaandaa na changamoto hiyo..katibu mkuu wa Kanisa la EAGT Mch.Brown Mwakipesile amesema kwamba
katibu mkuu wa Kanisa la EAGT Mch.Brown Mwakipesile |
"Ikiwa Yesu alipelekwa mahakani sisi ni kina nani hata tuogope kushitakiwa,,sisi kama EAGT tupo tayari kwa chochote ambacho Mungu ataruhusu kitupate''
Upya wa kesi hiyo hiyo iliyofunguliwa na TAG baada ya kupita miaka 21 tangu makanisa hayo yagawanyike kutoka Assemblies of God (AG) na kuwa Tanzania Assemblies of God na Evangelistic Assemblies of God ni ishara kmba ksa sasa TAG ina mtazamo mpya na kusudio thabiti la kuyadai makanisa hayo chini ya Askofu mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali tofauti na maaskofu waliotangulia.
Awali mapema mwezi huu September kauli ya Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali ilieleza kua
Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali |
"Mila za kiafrika mtu akizikwa pale pale panakua kwake .sasa tukasema kama tukikaa kimya hili likatokea baadae huko mbele tutasema nini tutajibu nini kwa sababu kanisa sio langu kanisa ni la general Council , Mimi nawajibika kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ,kwa wachungaji wote halafu sisi tutaondoka watakuja watoto hapa,wanataka kuchukua kanisa lao na kuna kaburi pale,Wasije watu wakachinjana hapo tupate muongozo wa kisheria ndio hilo tuu
Muongozo wa kisheria juu ya jambo hili jamani isije ikatokea confusion huko mbele,
Lakini nawaambieni ukweli hakuna mtu aliyefurahia kama mimi kwa mzee kulola kuzikwa Bugando mimi nimefurahi saaana naomba muandike hivyo ndugu waandishi nimefurahi saana Mzee kulola kuzikwa Tanzania Assemblies of God Bugando.
Sasa mzee kwa Heshima zote ameanza kazi Tanzania Assemblies of God mwaka 1968 mzee akaombwa na EAGT uongozi kwa busara yao kubwa na nzuri wameona alipoanzia ndio apumzishwe, amerudishwa nyumbani amerudishwa nyumbani baba yetu .
Mimi kama TAG na kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini lengo letu ilikua ni kuweka records tuu sawasawa kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo kuzuia maafa makubwa yanayoweza kutokea baadae.
Lakini haikua haswaa kuzuia Mzee Kulola kuzikwa pale Hata kesho tutakaporudishiwa lile jingo lile tutakaporudishiwa mahali petu kumiliki asilimia 100, mtu akitaka kuja kumuondoa pale mzee Kulola nyumbani, Mimi nitaweka stop order usimuondoe utamuondoa umpeleke wapi na mzee amelala nyumbani nitasema jamani hapana mwacheni mzee kulola amelala nyumbani.''