Habari kutoka nchini Cameroon zinasema Rais wa nchi hiyo Paul Biya ameagiza kufungwa kwa makanisa ya kiroho takribani 100 yaliyopo katika miji mikubwa nchini humo kwa madai ya kwamba wachungaji wa makanisa hayo wanaiweka katika hali ya hatari kiusalama nchi hiyo iliyoko Afrika magharibi.
Kwa mujibu wa wachungaji wa makanisa ya Kipentecoste nchini humo wamesema hatua hiyo ni kithibitisho kwamba Rais huyo hayuko salama kwa mwenendo wa makanisa hayo kuikosoa serikali yake, Biya kwakutumia vikosi vya jeshi amekuwa akiyafunga makanisa ya Pentecoste katika mji mkuu wa nchi hiyo Yaounde na mkoa wa kaskazini magharibi wa Bamenda ambao una waumini wengi wa dini ya Kikrsito nchini humo.
" Zaidi ya makanisa 50 yameshafungwa mpaka sasa, serikali inampango wa kuyafungia takribani makanisa 100 katika miji nane nhini humo.
Msemaji mmoja wa serikali katika mji wa Bamenda aliyefahamika kwa jina la Mbu Anthony ameiambia CNN kuwa watahakikisha wanaondoa makanisa yote ya kiroho ambayo wanaharibu jina la Yesu wakifanya miujiza feki na kuua wananchi katika makanisa yao, wameongeza uhuru tuliokuwa tumewapa, takribani makanisa 500 ya kiroho yamekuwa yakiendesha shughuli zao nchini humo ambapo kati yao ni 50 tu ndio yapo kihalali amesema Mbu Anthony.
Siku ya jumapili, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9 alianguka na kufariki dunia wakati wa maombi katika kanisa la Winner's Chapel lililopo mji wa Bamenda, ambapo mama mzazi wa mtoto huyo Mih Theresa ameiambia CNN siku ya jumatano kuwa wachungaji walikuwa wanajaribu kumtoa mapepo yaliyokuwa yamemjaa binti yake
" Naitaka serikali kuwaondoa hawa wachungaji wanaotumia nguvu za ajabu kuwavutia wachungaji na kuwaua mamia kwa nguvu hizo. Watoto wangu wote wamekimbia kanisa letu la Katoliki kufuata miujiza, maajabu ", ameiambia CNN akizuia machozi yake.
Mkristo mwingine aliyefahamika kwa jina la Mveng Thomas amesema ndoa yake imevunjika bila kutarajia baada ya mmoja wa wachungaji wa makanisa hayo kumwambia mkewe kwamba yeye ni mtenda dhambi mwakilishi wa shetani. Wachungaji wameandamana kupinga uamuzi huo wa serikali siku ya jumatano katika miji ya Bamenda na Douala, nakuongeza kuwa Rais huyo aliyepo madarakani toka mwaka 1982 amekuwa na wasiwasi na ukuaji wa makanisa nchini humo akihofia usalama wa serikali yake.
Kwa upande wa askofu Boniface Tum wa kanisa la Mungu jijini Yaounde amesema uhuru wa kuongea uliopo ndani ya makanisa hayo umemfanya awe na wasiwasi nayo sana hivyo kuamua kuyapa kibali makanisa ya Katoliki,Baptist, Presbyterian, Waislamu pamoja na baadhi ya makanisa, hali hiyo imewafanya wakristo katika mji wa Bamenda ambao makanisa yao yako kwenye hatari ya kufungiwa kuamua kugeuza kisiri nyumba zao kuwa makanisa.
source:gospelkitaa
Rais Paul Biya |