Mwanamuziki wa Nyimbo za injili nchini Tanzania anayekwenda kwa jina la Neema Gasper anatarajia kuachia kufanya tamasha kubwa la Gospel na kuzindua album yake mpya kabisa ya kwanza yenye nyimbo nane za Injili, uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika siku ya tarehe September 1, mwaka huu 2013 kuanzia mishale ya saa saba mchana katika ukumbi wa Ubungo Plaza
Tofauti na namna ilivyozoeleka katika uzinduzi wa album mbalimbali za wanamuziki wa gospel Uzinduzi huu wa album ya Shujaa unakuja kwa style ya kipekee ambapo kutakua na pambano la ngumi pamoja , Fashion show na mashindano ya Dancing.
Akiongea mbele ya wanahabari mwanamuziki Neema Gasper ameeleza kua mapato yatakayopatikana katika uzinduzi huo asilimia fulani ya mapato itapelekwa kusaidia wajane na yatima waishio katika mazingira magumu
Waimbaji wengine wa nyimbo za injili watakaomsindikiza Neema gasper katika uzinduzi wa album yake ni pamoja na Rose Mhando,Bahati Bukuku,Madam Ruth, Martha Mwaipaja, Everine Msoma, Ambwene Mwasongwe, Maxmillian Machumu, Edson Mwasabwite Enock Jonas na wengine wengi.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo anatajiwa kua Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Samuel Sita ambaye ataongoza jopo la wageni wengine waalikwa kumuunga mkono mwanamuziki huyo.
Album hii ya Shujaa itakua na nyimbo nane ikiwa ni pamoja na : Shujaa, Mweleze Yesu, Machozi yako, Nimekukimbilia Bwana,Ee Mungu,Kristo, Faida, na Kwa Neema.
Viingilio katika uzinduzi huo vimepangwa kua Viti maalum sh 10,000/=, Kawaida Wakubwa sh 5000/= na watoto sh 2000/=
na wageni 50 wa kwanza watajipatia mafuta na Losheni kutoka kwa Gress Product
Ticket zinapatikana Praise Power Radio,Wapo Radio, na pia ticket pia zitapatikana mlangoni siku hiyo hiyo ya uzinduzi katika ukumbi wa Ubungo plaza.
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Neema Gasper |
Akiongea mbele ya wanahabari mwanamuziki Neema Gasper ameeleza kua mapato yatakayopatikana katika uzinduzi huo asilimia fulani ya mapato itapelekwa kusaidia wajane na yatima waishio katika mazingira magumu
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Neema Gasper |
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo anatajiwa kua Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Samuel Sita ambaye ataongoza jopo la wageni wengine waalikwa kumuunga mkono mwanamuziki huyo.
Mh Samuel Sita, waziri wa ushirikiano wa afrika Mashariki |