Katika hali isiyokua ya Kawaida Mwanasheria Dola Indidis kutoka Kenya ameibuka na mashtaka dhidi ya utawala wa Israel na Italia kwa mateso na kifo cha Bwana Yesu kristo yaliyotokea miaka elfu mbili iliyopita.
Walalamikaji wamezitaja nchi za Italia na Israel kwakuwa nchi hizo hata baada ya uhuru zimeendelea kutumia sheria za Utawala wa Roma na zile zilitotumika kumsulubu msalabani Yesu.
Padri Mkuu wa Wayahudi Caiaphas anatuhumiwa kumkamata Yesu, kumshtaki kwenye mahakama isiyo halali (Kangaroo Court), na kumtia hatiani kwa mashtaka ya kidini yaliyoangukia kwenye adhabu ya kifo na hakutaka Yesu ahoji mamlaka yake.
Alidai Pilato hakumtia hatiani Yesu, lakini alitoa hukumu ya kumuua ili kuleta amani.
“Haikuwa sahihi Pilato kushuhudia mtuhumiwa akipigwa,” alisema Indidis na kuongeza kuwa, “Jaji lazima alisimamie haki za watu wote na aina zote za ukiukwaji wa sheria.”
“Miongoni mwa waliokuwepo walimshambulia usoni, walimtemea mate, walimzaba vibao, walimdhihaki, na kumwona kuwa mtu anayestahili kifo,” alisema.
Mlalamikaji pia alihoji mfumo wa maswali yaliyotumika wakati wa kesi, uchunguzi, wakati kesi ikisilikizwa na hukumu kwa Yesu Kristo, adhabu alizokuwa akipewa wakati kesi ikiendelea na ukweli wa taarifa zilizotumika kumtia hatiani. Alisema kilichofanyika ni uvunjaji wa haki za binadamu. “Yesu alikuja duniani kama binadamu. Sasa hakupewa fursa ya kusikilizwa na hakuna aliyezungumza kwa niaba yake.”
Indidis alisema ametumia miaka 10 kuifanyia kazi kesi hiyo, ikiwamo kukusanya ushahidi kutoka kwenye Biblia. “Ushahidi wote umo kwenye kumbukumbu za Biblia, huwezi kuidharau Biblia,” aliongeza Indidis.
Alisisitiza kwamba hata baada ya Yesu kufa, haikutolewa nafasi yoyote kusikilizwa kwa rufaa ya aina yoyote, hivyo yeye ameamua kufanya hivyo akiwa kama ‘rafiki’.
Alizungumza kuhusu kesi hiyo, mmoja wa maofisa wa ICJ alisema mahakama hiyo haina mamlaka kuhusiana na kesi ya aina hiyo kwa sasa kwa kuwa inajihusisha zaidi na kesi baina ya nchi na nchi, hivyo ni vigumu kuishughulikia kesi ya aina hiyo.
Source: Mwananchi
Walalamikaji wamezitaja nchi za Italia na Israel kwakuwa nchi hizo hata baada ya uhuru zimeendelea kutumia sheria za Utawala wa Roma na zile zilitotumika kumsulubu msalabani Yesu.
Mwanasheria wa Kenya Dola Indidis |