Mwanamuziki wa nyimbo za injili anayekuja kwa kasi kubwa nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Josephine Minza hivi karibuni anatarajia kuachilia Live Video album yake mpya kabisa yenye nyimbo kumi ,inayokwenda kwa jina "Maisha ya Ibada" uzinduzi utakaofanyika September 22, mwaka huu 2013 majira ya saa nane mchana ndani ya kanisa la CCC upanga jijini Dar es Salaam.
Akiongea mbele ya wanahabari katika mkutano wake kwa waandishi wa habari Mwanamuziki Josephine Minza ameeleza kua album hii inakua album yake ya pili ambayo ndani yake kuna vionjo vingi ambavyo vimeongezwa ili kuipamba album hiyo.
Awali mwanamuziki huyo alishatoa album nyingine iliyokwenda kwa jina la Nakuabudu Bwana ambayo pia ilifanya vizuri kwa kugusa maisha ya watu wengi kupitia uimbaji wake.
Katika uzinduzi wa Album yake hii ya sasa Mwanamuziki Josephine Minza anasindikizwa katika uimbaji na wanamuziki mbali mbali wa Gospel ikiwa ni pamoja na Abednego Hango (wa New Life Band),Ipyana Kibona, Prisca Kangi, David Yona na Jenifar Mushi.
Album hii yenye jina Maisha ya Ibada imepikwa chini ya mtayarishaji mahiri wa muziki wa gospel kwa sasa nchini Tanzania bwana Samuel Yona ambapo katika maelezo yake bwana Yona ameeleza kuwa album hii imebeba vionjo mbalimbali vya kimuziki ambavyo kwa pamoja vimepikwa vizuri na kuifanya album hiyo kua ya aina yake ikiwa ni pamoja na vionjo vya Kwaito, Regae, na Slow Music.
Wakati huo huo mlezi wa huduma hii ya muziki na mratibu wa uzinduzi wa album hii anayefahamika kwa jina Mwalimu Mgisa Mtebe ameeleza kwamba mpaka sasa maandalizi yote ya uzinduzi huo yameshakamilika na siku hiyo wanatarajia kugusa maisha ya watu wengi na kuachilia uwepo wa Mungu utakaobadilisha mitazamo ya wengi na kuwafanya waishi maisha ya Ibada siku zote.
"kusudi kuu la Mungu kumuumba mwanadamu tangu awali ilikua ni kwa ajili ya mwanadamu amuabudu Mungu, lakini watu wengi wameacha kuishi kwa kufuata lengo hilo kuu la Mungu na kuishi maisha ya michanganyo, hivyo basi kupitia album hii na uzinduzi huu tunaokwenda kuufanya tunatarajia kuyabadilisha maisha ya watu wengi na kujenga madhabahu ya Ibada ndani ya mioyo ya wengi na kuwafanya wamuabudu Mungu muda wote kutoka mioyoni mwao.alisema Mtebe
Katika uzinduzi wa album hiyo hakutakua na kiingilio chochote,na wito umetolewa kwa wakazi wote jiji la Dar es Salaam kuhudhuria uzinduzi huo ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa shughuli hiyo wameeleza kuwa kila atakayehudhuria Ibada hiyo hatatoka kama alivyoingia kutokana na uwepo wa Mungu utakao kuwepo siku hiyo.
Unaweza kutazama sehem ya album hiyo wakati inarecodiwa kwa kubofya hapo chini
Akiongea mbele ya wanahabari katika mkutano wake kwa waandishi wa habari Mwanamuziki Josephine Minza ameeleza kua album hii inakua album yake ya pili ambayo ndani yake kuna vionjo vingi ambavyo vimeongezwa ili kuipamba album hiyo.
Awali mwanamuziki huyo alishatoa album nyingine iliyokwenda kwa jina la Nakuabudu Bwana ambayo pia ilifanya vizuri kwa kugusa maisha ya watu wengi kupitia uimbaji wake.
Mwanamuziki Josephine Minza Nkila |
Sehem ya picha ilivyokua wakat wa Live recording ya album hiyo |
Mtayarishaji mahiri wa muziki wa gospel kwa sasa nchini Tanzania bwana Samuel Yona |
Mwalimu Mgisa Mtebe kushoto akiwa na Josephine Minza wakifafanua jambo kwa waandishi wa habari |
sehem ya picha wakati wa Live Recording ya album hiyo |