Mlipuko mkubwa wa kitu kinachoaminika kua ni Bomu umetokea asubuhi ya leo katika kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi parokia ya Olasiti jijini Arusha wakati ibada ya uzinduzi wa kanisa hilo ikiwa inaendelea ambapo mgeni rasmi kutoka Vatican alikua Balozi wa Papa Francis 1
Idadi ya majeruhi hadi hivi sasa ni 60 huku mtu mmoja akiripotiwa kupoteza maisha kutokana na mlipuko huo..
Jeshi la Polisi linamshikiria mtu mmoja akihusishwa na tukio hilo..
Kanisa hilo la Mt.Joseph Mfanyakazi parokia ya Olasiti ni kanisa lililojengwa kwa jitihada ya waumini ambao walijichanga kwa pamoja na kuweza kulijenga kanisa hilo na siku ya leo Uzinduzi wa kanisa hilo ndio ulikua ukiendelea ambapo Balozi wa papa alikua ndie Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo...
kwa mujibu wa chanzo kimojawapo cha habari imeelezwa kuwa Mlipuko huo umetokea mapema asubuhi ya leo majira ya saa nne na nusu asubuhi wakati Ibada ya uzinduzi wa kanisa hilo ikiwa inaendelea huku tendo la Kubariki maji ndio lilikua likiendelea ndipo wakatokea watu kwa gari eneo hilo na kisha kurusha kitu kinachosadikiwa kua ni bomu katika kanisa hilo
Jeshi la Polisi linamshikiria mtu mmoja akihusishwa na tukio hilo..
Kanisa hilo la Mt.Joseph Mfanyakazi parokia ya Olasiti ni kanisa lililojengwa kwa jitihada ya waumini ambao walijichanga kwa pamoja na kuweza kulijenga kanisa hilo na siku ya leo Uzinduzi wa kanisa hilo ndio ulikua ukiendelea ambapo Balozi wa papa alikua ndie Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo...
RPC mkoa wa Arusha ametoa hotuba yake na kusema ni tukio la kigaidi, pia amesema wanawasaka wote waliohusika na tukio hilo na ameomba watanzania wawe watulivu wakati wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Uzinduzi wa kanisa hilo la Mtakatifu Joseph parokia ya Olasiti umesitishwa hadi hapo utakapotangazwa baadaye.
Uzinduzi wa kanisa hilo la Mtakatifu Joseph parokia ya Olasiti umesitishwa hadi hapo utakapotangazwa baadaye.
Tutaendelea kukuhabarisha kwa taarifa zaidi kadri zitakapotufikia