Hatimaye kesi iliyokua inamkabili Mchungaji Creflo Dollar kwa mashitaka ya kumjeruhi Binti yake ,imemalizika huku mchungaji huyo akitakiwa kulipa faini ya dola za kimarekani zipatazo 1,072.kama gharama za uendeshaji wa kesi hiyo mahakamani .
Mnamo june 7 mwaka 2012 Mchungaji Creflo Dollar mwenye umri wa miaka 50,kiongozi wa kanisa la World Changers International chini Marekani alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kumjeruhi mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 15 kwa kile kilichoelezwa kuwa ilikua ni katika mabishano na binti yake baada ya kumzuia binti huyo asitoke kwenda kwenye party iliyokua ifanyike usiku huo.
Creflo Dollar aliachiliwa kwa dhamana ya dola za kimarekani zipatazo 5000 huku akitakiwa kuripoti mara kwa mara katika mahakama.
Kwa mujibu wa Alexandria Dollar mwenye umri wa miaka19 mtoto mwingine wa mchungaji Creflo Dollar alieleza kwamba katika tukio hilo alishuhudia baba yake akimkaba shingo mdogo wake kwa sekunde 5, na kumchapa makofi yaliyomdondosha chini na kumsababishia maumivu binti huyo.
Nyumba anamoishi Mchungaji Creflo Dollar na familia yake |
Akitoa maelezo yake kwa officer mmojawapo wa mahakama mchungaji Creflo Dollar alisema kwamba tabia ya binti yake ilianza kubadilika na kuwa na utovu wa nidhamu ambapo alieleza kuwa katika mabishano hayo binti huyo alithubutu hadi kumchapa kibao baba yake (mch.Creflo Dollar) kitendo kilichoamsha hasira na kuchukua hatua ya kumuadhibu binti huyo.
Akielezea tukio hilo mchungaji Creflo Dollar alisema
“Nikiwa kama baba ,
Ninawapenda sana
watoto wangu na
marazote kutoka
moyoni mwangu
ninawatakia mema
na mafanikio katika
maisha yao,hivyo binafsi
siwezi kutumia mkono
wangu kumsababishia
maumivu mtoto wangu
hata kidogo
Ninawapenda sana
watoto wangu na
marazote kutoka
moyoni mwangu
ninawatakia mema
na mafanikio katika
maisha yao,hivyo binafsi
siwezi kutumia mkono
wangu kumsababishia
maumivu mtoto wangu
hata kidogo
Katika kesi hiyo tume iliundwa kufatilia mwenendo wa mchungaji huyo hususan katika suala zima la ku control Hasira za mchungaji huyo, tume hiyo ilidumu kwa takriban miezi mitatu ikimtaka mchungaji huyo kuripoti mara kwa mara kwa afisa wa Mahakama kwa matazamio.ambapo katika kipinchi chote hicho hakutakiwa kufanya kosa lolote.
Hivi karibuni tume hiyo ilimaliza kazi yake na kusema kua mchungaji huo hajafanya kosa lolote katika kipindi hicho chote alichowekwa katika uangalizi hivyo mashtaka yote yaliyokua yanamkabili yameondolewa na anachotakiwa ni kulipa fidia za uendeshaji wa kesi hiyo tu
Kujua alichokisema mchungaji huyo kuhusu kesi hiyo tazama video hapa chini