Mchungaji Yousef Nadarkhani aliyewahi kuhukumiwa adhabu ya kifo na baadae kuachiliwa na mahakama ya rufaa nchini Iran kutokana na kupatikana na hatia ya makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za uinjilishaji na ukristo nchini humo amerudishwa tena Gerezani siku chache kabla ya Christmas 2012.
picha inayoonesha namna waliohukumiwa kunyongwa inavyokua waka wa kutelezwa adhabu hiyo |
Mchungaji Yousef Nadarkhani |
Kwa mujibu wa taasisi ijulikanayo kama Christian Solidarity Worldwide (CSW) imesema kwamba Mchungaji Nadarkhan amerudishwa gerezani kwa mara nyingine tena kwa amri iliyotolewa na mkuu wa gereza la Lakan, akidai kwamba Mchungaji Nadarkhan aliachiliwa gerezani mapema kabla ya wakati, kutokana na shinikizo la mwanasheria wake Mohmmed Ali Dadkhah.
Mnamo mwezi september mwaka huu 2012 taasisi ijulikanayo kama Christian Solidarity Worldwide (CSW) iliripoti kuachiliwa kwa mchungaji huyo na kuthibitisha kwa kuonesha picha zinazomuonesha mchungaji huyo akitoka gerezani siku ya jumamosi ya tarehe 8september 2012 na kuungana na familia yake baada ya kutengana nayo kwa miaka mingi.
Moja ya picha zilizotolewa zikimuonesha Mchungaji Nadarkhan akiwa anatoka gerezani na kuungana na familia yake |
Mchungaji Nadarkhan akiungana na mkewe mapema mwezi september mwaka huu 2012. baada ya kuachiliwa toka Gerezani |
kutokana na makosa hayo mwaka 2010 nchi ya Irani ilitoa adhabu ya kifo kwa mchungaji huyo kunyongwa hadi kufa kutokana na kukutwa pia na makosa mengine akifanya shughuli za uinjilishaji na kuhubiri injili ya Yesu kristo katika nchi hiyo ambayo ni nchi ya kiislam na inayoongozwa kwa sheria za kiislam.
Katika mahakama ya nchi hiyo siku ya tarehe 8september mwaka huu 2012 kesi ya Nadarkhan ilidumu kwa muda wa masaa sita lakini mwisho mahakama hiyo ilimuachilia huru Mchungaji Nadarkhan.
awali wakati anaachiliwa toka gerezani mtandao wa ujulikanao kama ACJL ambao ulizindua kampeni kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuishinikiza serikali ya Iran kumwachilia mchungaji huyo, pia ulisema kwamba Nadarkan alikutwa na makosa ya kufanya Uinjilist kwa Waislam kosa ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo ni kifungo cha miaka mitatu jela hivyo kwa kipindi chote cha miaka mitatu ambacho mchungaji huyo alikaa gerezani mda wa kifungo hicho ulishamalizika.
katika kipindi chote alichokua uraian baada ya kuachiliwa toka gerezan Nadarkhan amekua akihojiwa mahali pengi ikiwa ni pamoja na November mwaka huu ambapo Nadarkhan alikuwa mgeni wa heshima katika CSW’s National Conference jijini London, England, na kuwashukuru wote waliokua wakimuombea kipindi chote alichokuwa gerezani hadi kuachiliwa kwake.
Mervyn Thomas, Mkurugenzi wa taasisi ya (CSW) Christian Solidarity Worldwide |
Mervyn Thomas, |
“We are disappointed to hear Pastor Nadarkhani has been returned to prison in such an irregular manner. The timing is insensitive and especially sad for his wife and sons, who must have been looking forward to celebrating Christmas with him for the first time in three years.
“We hope that Pastor Nadarkhani will be released without delay once this alleged sentence has been fully served. We are also asking for prayers for the pastor's safety, and for his family at this difficult time.”