Kongamano kubwa la Wanaume lafanyika kwa mara ya kwanza ndani ya National Museum Theater jijini Dar es Salaam,Kongamano hilo lililoanza siku ya tarehe 19 November hadi 25November mwaka huu 2012 kuanzia saa kumi na moja na nusu jioni hadi saa mbili na nusu usiku linawakutanisha watu mbali mbali kwa lengo la kujadili changamoto zinazomkabili Mwanaume katika kumtumikia Mungu,na katika mafanikio yake ndani ya jamii inayomzunguka.
Kongamano hilo likiwa na kauli "Haki uvamizi wa Kweli
( Righteous Invasion of Truth R.O.T) furaha huleta mashujaa" linafanyika kama jukwaa linalowakutanisha wanaume toka katika makundi mbali mbali tofauti ya kikabila,kijamii,kiuchumi na kidini kwa lengo la kumrejesha,kubadili, kumuandaa, na kumsaidia mwanaume kwa ujumla katika nyanja zote za kimaisha.
Miongoni mwa mambo yanayojadiliwa katika kongamano hilo ni changamoto zinazowakabili wanaume ikiwa ni pamoja na tabia ya wanaume walio wengi kuficha mambo yao siri bila kumshirikisha mtu yoyote ilihali yanawatesa kwa ndani,
Mambo mengine ni pamoja na changamoto zinazomkabili mwanaume katika familia,masuala ya kiafya hususan athari zinazowakabili wanaume wanaotumia vilevi i.e Pombe na sigara, hali inayopelekea ongezeko kubwa la kwa idadi ya vifo kwa wanaume kulinganisha na idadi ya vifo kwa wanawake.
Kongamano hili la Wanaume mwisho litatoa mbinu mbali mbali kama suluhisho la matatizo hayo hususan katika mlengo unaotokana na neno la Mungu na kumfanya mtu aweze kumuabudu Mungu huku nafsi na roho yake ikiwa huru mbali na changamoto mbalimbali za kimaisha.
Sehem ya watu waliohudhuria katika kongamano hilo linalofanyika National Museum Theater jijini Dar es Salaam |
( Righteous Invasion of Truth R.O.T) furaha huleta mashujaa" linafanyika kama jukwaa linalowakutanisha wanaume toka katika makundi mbali mbali tofauti ya kikabila,kijamii,kiuchumi na kidini kwa lengo la kumrejesha,kubadili, kumuandaa, na kumsaidia mwanaume kwa ujumla katika nyanja zote za kimaisha.
Miongoni mwa mambo yanayojadiliwa katika kongamano hilo ni changamoto zinazowakabili wanaume ikiwa ni pamoja na tabia ya wanaume walio wengi kuficha mambo yao siri bila kumshirikisha mtu yoyote ilihali yanawatesa kwa ndani,
Mambo mengine ni pamoja na changamoto zinazomkabili mwanaume katika familia,masuala ya kiafya hususan athari zinazowakabili wanaume wanaotumia vilevi i.e Pombe na sigara, hali inayopelekea ongezeko kubwa la kwa idadi ya vifo kwa wanaume kulinganisha na idadi ya vifo kwa wanawake.
Kongamano hili la Wanaume mwisho litatoa mbinu mbali mbali kama suluhisho la matatizo hayo hususan katika mlengo unaotokana na neno la Mungu na kumfanya mtu aweze kumuabudu Mungu huku nafsi na roho yake ikiwa huru mbali na changamoto mbalimbali za kimaisha.
Baadhi ya vikundi vya uimbaji vinavyohudumu katika Kongamano hilo ndani ya National Museum Theater Dar es Salaam |