Serikali ya Msumbiji imeingiza sheria mpya inayoyataka makanisa nchini humo kuanza kulipa kodi kwa serikali kama taasisi zingine za kibiashara .
Kodi hiyo itayahusu makanisa yote nchini humo hususan makanisa yote ambayo yanajishughulisha na shughuli na miradi mbalimbali ya kiuchumi katika kujiongezea kipato kwa makanisa hayo.
Maeneno mengine yatakayotozwa kodi katika makanisa hayo ni pamoja na sadaka zitakazokuwa zinapatikana kutoka katika makanisa nchini humo.
Serikali ya Msumbiji imeamua kuweka sheria hii kwa kudai kuwa makanisa nchini humo yanajiendesha kwa faida kutokana na mapato yanayopatikana makanisani humo kama taasisi zingine za kibiashara nchini humo zinavyojiendesha hivyo makanisa pia hayana budi kulipa kodi kwa serikali ili kukuza uchumi wa nchi ya Msumbiji.
Kutokana na sheria hiyo kumezuka sintofaham huku wadau mbali mbali wakisema kuwa kuingiza sheria hiyo ni sawa na kuvunja misingi ya Neno la Mungu, huku wadau wengine wakidai yaliyo ya kaisari mpeni kaisari na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu.....
Kama umeguswa na na habari hiii unaweza kutoa maoni yako kuhusu habari hii kwa kuingia hapo chini kwenye kitufe cha Comments kisha andika maoni yako.