Jackson Benty Kuongoza Tamasha la Kusifu na Kuabudu Mabibo Hostel
Jumamosi hii na jumapili ya tarehe 12-13/05/2012 kutafanyika Tamasha la Muziki wa Injili pamoja na Mafundisho ya NENO LA MUNGU katika huduma ya EN-EGLAIM MINISTRY inayoongozwa na Mtumishi wa Mungu AGNESS MALYA iliyoko Mabibo Hostel jijini Dar es salaam.
Katika tamasha hilo ambalo litajumuisha waimbaji wakubwa kwa wadogo linatarajiwa kuanza kuanzia saa 8:00 Mchana mpaka 12jioni ambapo mtumishi wa Mungu Jackson Benty pamoja na Enock Jonas ni miongoni mwa wanamuziki wa injili watakaomtukuza Mungu mahali hapo.
Pamoja na Tamasha hilo kutakuwepo na Mafundisho maalumu
Wale wote wanaopitia Changamoto za Ndoa
Wale wote wenye ndoto ya kumtumikia Mungu