BORA UKOSEE KUJENGA, KULIKO KUKOSEA KUOA!!!
Brother nakushauri kama ndugu na rafiki yako, usiingie kwenye NDOA na mtu kwasababu unamhurumia, ni kosa kubwa sana.
Yaani kila ukichunguza moyoni mwako unaona kabisa humpendi, au unampenda ule upendo wa kirafiki sio wa mke na mume, lakini unakaza eti kisa mmetoka mbali, sijui amekusaidia mambo mengi, mara watu wanawafahamu mmekuwa pamoja siku nyingi, sijui anajulikana na ndugu zako. Hizo sababu zote hazina msingi kama humpendi kutoka ndani kwenye vilindi vya moyo wako.
Hata kama watu wanakushauri mnaendana, kumbuka huolei watu. Hao watu wanaishia ukumbini siku ya harusi baada ya hapo mziki wa maisha na huyo mrembo utaucheza mwenyewe.
Unaweza kuwa na mtu ambaye ukiangalia hana kasoro yeyote, anakila kitu ambacho watu wanatafuta na kutamani lakini ukichunguza ndani yako ile nafasi ya mke hafit, yaani hajazi kabisa, ndugu usijidanganye kuwa mtazoeana taratibu, kama haenei, haenei, usije kumtesa mototo wa watu. Ni bora kuliweka yai chini kwa usalama kuliko kulibeba na kisha ukaliachia kutoka juu, maana halitapona, lazima lipasuke.
Kuwa mwanaume “BE A MAN” mwambie ukweli, usimpotezee muda. Usizibie nafasi wenzio wenye malengo naye wakati wewe unajua kabisa hakuna mahali mnapokwenda. Mpe uhuru kutafuta mahusiano yenye future.
Muombe Mungu hekima, tumia lugha nzuri, mueleweshe kisha mpe uhuru atengeneze maisha yake, na wewe endelea na hamsini zako. Najua wadada wengi hawakubaligi ukweli huu hasa unapomwambia kuwa “huku ndani sioni kama wewe ni mke wangu” wapendwa wataanza na kulazimisha kuwa Mungu alisema nao, hayo yasikutishe.
Fanya maamuzi sahihi na maisha yako. Oa mtu unayejua hata afanyeje unampenda kutoka ndani, anaweza asiwe na mvuto kwenye macho ya watu wengine, ila kama ndio chaguo lako, potezea mitazamo ya watu, kamata chombo chako, fuata utaratibu, lipa mahali yote, funga ndoa, ingiza kifaa ndani kisha maisha yanaendelea.
USIJE KUOA MAJUTO, WALA USIISHI NA MTU KWA KUVUMILIA KULINDA AGANO, HAKIKISHA UNAMPENDA HATA AKIKUVURUGA UNAWEZA KUSAMEHE NA KUACHILIA. BORA UFANYE MAKOSA KATIKA UJENZI, UNAWEZA KUBOMOA, ILA USIKOSEE SUALA LA NDOA………ME NAKUSHAURI TU.