Mwanamuziki Israel Houghton wa nyimbo za injili kutoka nchini Marekani ameungana na maelfu ya wakazi wa Uganda katika Sherehe maarufu zilizopewa jina Watoto Big Party sherehe zilizofanyika katika viwanja vya kanisa la Watoto Kyengera jijini Kampala nchini Uganda
Sherehe hizo zimefanyika ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya miaka 30 tangu huduma ya Watoto kuanzishwa nchini Uganda, sherehe ambazo zilipambwa na mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa injili duniani Israel Houghton na kundi lake la New Breed kutoka nchini Marekani.
Wageni wengine waliohudhuria kilele hicho ni pamoja na mchungaji kiongozi na mwanzilishi wa kanisa la Hillsong duniani lenye makao makuu yake nchini Australia Brian na mkewe Bobby Houston, wageni mbalimbali pamoja na watu waliolelewa na huduma hiyo toka ilipoanzishwa pamoja na waumini wa kanisa la Watoto ambalo limekuwa maarufu duniani kutokana na kwaya ya Watoto ambayo hufanya ziara kila mwaka duniani
Matukio zaidi kuhusu Sherehe hizo zilizofana ni kama zinavyoonekana hapa katika picha chini
Mambo yalikua kama hivi inavyoonekana hapa |
Matukio zaidi kuhusu Sherehe hizo zilizofana ni kama zinavyoonekana hapa katika picha chini
Mwanadada Charlin Moore wa New Breed akisukuma sauti kumsifu Mungu. |
Israel Houghton |
sehemu ya umati wa watu uliohudhuria |
Waanzilishi wa huduma ya Watoto Gary na mkewe wakiwa wenye furaha. |
Watoto Children kwaya wakimsifu Mungu. |
Watoto Children kwaya wakiimba kwa furaha katika maadhimisho hayo. |
Mmoja wa watoto akiimba kwa hisia, moja ya kisa ni kwamba baadhi ya watoto wanaoishi kijijini humo baadhi yao wazazi wao waliuwawa na baba ya watoto wengine ambao pia wapo kijijini hapo, ila watoto wote wamesameheana. |
Vijana kutoka kanisa la Watoto wakiwajibika. |
Brian Houston wa Hillsong na mkewe pamoja na waanzilishi wa huduma ya Watoto mchungaji Gary Skinner na mkewe. |
Baadhi ya waimbaji waliokuwa upande wa kwaya kubwa. |
Kijiji cha Watoto ambacho kinatunza watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa ukimwi na ambao walifariki kwa vita kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo jumla ya nyumba 406 mpaka sasa zimejengwa kwenye kijiji hicho. ©Watotochurch |