Katika hali isiyokua ya kawaida wachungaji mjini Tabora wamejikuta matatani baada ya kumualika mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Tanzania Rose Mhando kwa lengo la kuperfom katika uzinduzi wa Album yake mwimbaji wa nyimbo za injili na mchungaji mmoja wa kanisa moja wapo mjini Tabora ajulikanaye kwa jina la Egon Israel na badala yake Rose Mhando kuingia mitini na hela ambayo alikua amekwisha lipwa na wachungaji hao kwa lengo la kuhudhuria na kuimba kwenye uzinduzi huo.
Kwa mujibu wa walalamikaji katika tukio hilo la kustaajabisha hususan katika mziki wa injili ambao kwa asilimia kubwa hua unahusianishwa sana na huduma ya kiroho zaidi kuliko biashara lakini hali ilikua tofauti ambapo Mwanamuziki Rose Mhando alikubaliana na wachungaji hao kwenda kuperfom kwenye uzinduzi huo kwa masharti ya kulipwa kiasi cha shilingi Milion 2 Kupitia akaunti yake Rose Mhando iliyopo NMB Bank, fedha ambayo wachungaji hao walitii ombi hilo na baadae kumlipa fedha hiyo kama walivyoelekezwa na mwanamuziki huyo.
Sinema hii ya aina yake ilianza kupamba moto pale ambapo mda wa tukio ulikua umewadia katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi na umati mkubwa wa watu waliolipia Viingilio walikua tayari wameshawasili wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Bi Fatma Mwasa ambaye alikua mgeni Rasmi katika tukio hilo na wakiwa na kiu ya kumuona mwanamuziki Rose Mhando akifanya vitu vyake stejini siku hiyo lakini kiu hiyo ilianza kuzorota baada ya mda uliopangwa kuanza kuyoyoma huku matumaini ya kumuona Rose Mhando yakififia Taratibu
Hali ilianza kua mbaya zaidi pale ambapo wananchi hao walianza kulalamika na kuanzisha vurugu wakidai kutapeliwa fedha zao za viingilio mbele ya mkuu wa mkuu wa mkoa ambapo awali walikua wametangaziwa ama kuahidiwa kuona show kali ya kukata na Mundu toka kwa gwiji la muziki Rose Mhando.
Kadri mda ulivyoanza kuyoyoma huku Rose Mhando akionekana kua ameingia mitini na fedha kiasi cha shilingi Milion 2 alizokua tayari ameshalipwa na wachungaji hao vurugu kubwa iliibuka hali iliyopelekea kikosi cha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuanza kutuliza ghasia hizo na kuwaokoa wachungaji hao
Hadi tunakwenda Mitamboni kiasi cha hasara kilichopatikana kutokana na Rose Mhando kuingia mitini na pesa za wachungaji hao bila kutoa taarifa yoyote iliyopelekea kutohudhuria uzinduzi huo kumepeleka kupatikana kwa hasara ya kiasi kisichopungua Milion 15 pesa za kitanzania huku wahudhuriaji wakirudishiwa Viingilio vyao.
Juhudi za kumtafuta Rose Mhando kujibu tuhuma hizo ziligonga Mwamba baada ya simu yake kutopatikana hewani kwa muda flani na kila ilipopatikana ikawa haipokelewi hali iliyopelekea pia kuongeza hofu na maswali zaidi ya elfu moja pasipo majibu ikiwa ni sababu zipi hasa zilimpelekea Rose Mhando kuingia mitini na kiasi hicho cha Pesa za wachungaji hao bila kutoa maelezo yoyote ya kuridhisha.
Hii si mara ya kwanza kwa kesi kama hiyo kuripotiwa ikimtuhumu mwanamuziki Rose Mhando kulipwa hela na kuingia mitini bila kutoa taarifa zozote. kesi kama hiyo iliwahi kutokea Arusha na Geita pia ikiwa na mazingira yanayofanana yanayohusishwa na aina moja wapo ya utapeli.
Mwanamuziki Rose Mhando |