Wadau mbalimbali wamekutana pamoja ikiwa ni katika hatua za mwanzo za maandalizi ya Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu lenye chimbuko lake nchini Kenya na baadae kusambaa katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki ambapo Tanzania ni moja wapo ya nchi ambapo Tamasha hili hufanyika kila Mwaka likiwa na ujumbe mkuu Africa Let's Worship (AFLEWO).
Katika maandalizi ya Awali ya Tamasha hilo wachungaji mbalimbali toka madhehebu mbalimbali ya kiroho walipata wasaa wa kukaa pamoja na kujadili mambo mbali mbali ili kulifanya tamasha hili liwe na ubora stahiki utakao mpa Mungu Utukufu na pia kuwahamasisha watu wengi zaidi wapate kukusanyika siku hiyo na kumuabudu Mungu kwa pamoja.
Miongoni mwa wadau waliokutana mapema wiki hii ni pamoja na Walezi wa huduma ya AFLEWO Tanzania ambao ni Pastor Paul Safari (DPC), Bishop Fredrick Kyara (P.C.E.A St. Columbus), Mwenyekiti Geoffrey Obielo na Administrator wa AFLEWO Tanzania Anna Abella Munyagi.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kutoa wito kwa wachungaji mbalimbali kuweka tofauti zao pembeni na kuwaruhusu waimbaji kutoka katika makanisa yao ili waweze kushiriki kikamilifu katika kulifanikisha tamasha hili kwa kujitoa kwa moyo katika kipindi chote cha maandalizi,mazoezi ya uimbaji mpaka siku yenyewe ya Tamasha litakapofanyika
Aidha wito pia umetolewa kwa wachungaji kuwapa nafasi Mass Choir ya Aflewo itakayoundwa siku chache zijazo kuweza kuanza kufanya huduma za kusifu na kuabudu katika makanisa tofauti tofauti katika siku za usoni kabla ya mkesha wa Aflewo ikiwa ni katika kulitangaza tamasha hilo na kuwafikishia taarifa watu wengi zaidi ili waelewe tamasha hilo na pia waweze kuhudhuria kwa wingi siku ya Tamasha litakapofanyika
Kikao hiki kinafanyika ikiwa ni siku chache zimebaki kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa kwa waimbaji na wanamuziki na wahudumu wa Tamasha hilo usajili unaotarajiwa kuanza kufanyika siku ya jumapili hii tarehe 17November 2013 katika kanisa la City Christian Center (CCC) na zoezi hilo kufungwa mwezi january mwaka 2014 Kisha mazoezi kwa Mass Choir kuanza rasmi.
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania AFLEWO ilifanyika mwaka 2011 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo baadae mwaka 2012 tamsha hilo likafanyika katika kanisa la City Christian Centre (CCC) Upanga, na mwaka huu AFLEWO 2013 ilifanyika katika Kanisa BCIC Mbezi Beach, na mwaka 2014 Tamasha hilo linategemewa kufayika mwezi wa sita ambapo mpaka sasa bado Eneo tamasha hili litakapofanyikia bado haijatangazwa rasmi.
Mlezi wa AFLEWO Tanzania Bishop Fredrick Kyara (P.C.E.A St. Columbus), |
Mlezi wa AFLEWO Tanzania Pastor Paul Safari (DPC) |
Miongoni mwa wadau waliokutana mapema wiki hii ni pamoja na Walezi wa huduma ya AFLEWO Tanzania ambao ni Pastor Paul Safari (DPC), Bishop Fredrick Kyara (P.C.E.A St. Columbus), Mwenyekiti Geoffrey Obielo na Administrator wa AFLEWO Tanzania Anna Abella Munyagi.
Watumishi wa Mungu mbalimbali wakiwa makini kumsikiliza mzungumzaji katika kusanyiko hilo |
Kikao hiki kinafanyika ikiwa ni siku chache zimebaki kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa kwa waimbaji na wanamuziki na wahudumu wa Tamasha hilo usajili unaotarajiwa kuanza kufanyika siku ya jumapili hii tarehe 17November 2013 katika kanisa la City Christian Center (CCC) na zoezi hilo kufungwa mwezi january mwaka 2014 Kisha mazoezi kwa Mass Choir kuanza rasmi.
Pastor Fred Okello kutoka Upper Roo Ministry,Pembeni ni ni mchungaji mwakilishi kutoka Mlima wa Moto kwa Mama Rwakatare Mikocheni B. |
Mama Shegga |
Bishop Mwende toka DPC |
picha kwa hisani ya Tunu Bashemela