Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,amefanya ziara ya ghafla kumtembelea Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Machui, na kumpa pole,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni |
Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja. |