Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Tanzania ,John Lissu October 6 mwaka huu 2013 anatarajia kurekodi
tena album ya pili yenye jina "UKO HAPA "itakayo rekodiwa katika Ukumbi wa kanisa la City Christian Center (CCC) Upanga jijini Dar es salaam album ambayo inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika muziki wa injili nchini Tanzania na kutoa hamasa kwa waimbaji wengine na kwaya mbalimbali kuanza kupenda kufanya kazi zinazorekodiwa LIVE.
Mwanamuziki John Lissu ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Singida,Tanzania ni kijana aliyejaaliwa sauti ya ajabu, alianza kujulikana alipofanya album yake live ya 'Jehovah yu hai' ambayo inanyimbo nzuri sana na album ya kwanza kurekodiwa LIVE yaani audio na Video kwa pamoja.
Baada ya hapo
amefanya kazi na kanisa la DPC akiwa mstari wa mbele kuongoza watu
katika sifa na kuabudu. Alishiriki pia katika recording ya Sifa zivume,
album nyingine iliyorekodiwa LIVE katika Ukumbi wa Mlimani City.
John Lisu amesema kuwa albam hii pili yenye jina "Uko Hapa" ina jumla ya Nyimbo 11 ambazo zitarekodiwa live siku hiyo pia ameongeza kua aliamua kuipa jina albam hiyo la "Uko Hapa" kwa sababu kila wakati ambapo Lissu amekuwa akihudumu Mungu amekuwa hapo akihudumia watu wake.
Mwanamuziki John Lissu ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Singida,Tanzania ni kijana aliyejaaliwa sauti ya ajabu, alianza kujulikana alipofanya album yake live ya 'Jehovah yu hai' ambayo inanyimbo nzuri sana na album ya kwanza kurekodiwa LIVE yaani audio na Video kwa pamoja.
John Lisu akiwa na timu yake katika maandalizi ya Live Recording ya Album yake mpya |
John Lisu amesema kuwa albam hii pili yenye jina "Uko Hapa" ina jumla ya Nyimbo 11 ambazo zitarekodiwa live siku hiyo pia ameongeza kua aliamua kuipa jina albam hiyo la "Uko Hapa" kwa sababu kila wakati ambapo Lissu amekuwa akihudumu Mungu amekuwa hapo akihudumia watu wake.
Baadhi ya mavazi yatakayovaliwa siku hiyoo.... |