Mwili wa askofu mkuu wa kanisa la EAGT Dr.Moses Kulola umewasili mchana wa leo jijini Mwanza na kupokewa na maelfu ya wakazi wa mji huu wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo injinia Evarist Ndikiro pamoja na viongozi wa makanisa yote ya jijini Mwanza.
Ikiwa ni majira ya saa saba na dakika nane mchana kweupee,ndani ya airpot ya jiji la Mwanza Mwili wa askofu mkuu Dr.Moses Kulola ukitokea Dar es salaam ukawasili ndani ya airpot ya jiji la Mwanza ukiwa katika ndege ndogo huku ukisindikizwa na viongozi wa kitaifa wa EAGT pamoja na mama mjane yani mke wa Askofu Kulola.
Mwili huo ukalakiwa na umati mkubwa sana wa wakazi wa jiji la Mwanza waliokua wamejipanga airpot huku wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Egeneer Evarist Ndikiro akiambatana na mkuu wa Usalama mkoa wa Mwanza Mwalim Jackob Mutashi.
baada ya kuwasili kwa mwili maelfu wakampokea baba wa kiroho wa kanisa la Tanzania Askofu Moses Kulola huku simanzi na majonzi mazito zikiwa zimegubika katika nyuso za kila mmoja aliyekuwepo uwanjani hapo.
Vilio vya uchungu sana vikasikika toka kwa kila mmoja aliyekuwepo uwanjani hapo huku kila mtu akitafakari moyoni mwake kwa namna alivyokua akiguswa na mahubiri na mafundisho toka kwa Askofu Moses Kulola shujaa wa injili nchini Tanzania
baada ya hapo msafara mkubwa sana ukaanza safari kutoka ndani ya uwanja wa ndege na kuelekea nyumbani alimokua akiishi Askofu Moses Kulola eneo la Capripoint jijini Mwanza.
wakati msafara huu ukianza kutoka uwanjani hapo majira ya saa saba na dakika ishirini na kuingia katika barabara ya mji huo kutoka airpot kuingia mjini kati mara ghafla wingu zito likaifunika Mwanza nzima na kufanya mazingira kuonekana kama ni jioni japokuwa ni mchana wa saa saba.
Wingu hilo likaendelea kufunika mji wa mwanza mda wote ambapo mwili huo ulipokua ukipita ukiwa umebebwa kwa gari dogo jeusi katika barabara ya kutoka airpot kwenda mjini kati mpaka eneo la Capripoint eneo alimokua anaishi Askofu Kulola ambapo baada ya mwili kufika nyumbani ghafla ikaanza kunyesha mvua kubwa sana katika jiji la Mwanza iliyoambatana na radi.
Picha na matukio zaidi hizi hapa chini

Add caption |