Mkuu wa mkoa wa Mwanza injinia Evarist Ndikiro akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu mkuu Moses Kulola |
sehemu ya umati wa watu waliohudhuria kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa baba wa kiroho Askofu Moses Kulola |
Misururu mirefu ya watu waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa askofu Moses Kulola |
Mwili wa Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT na baba wa kiroho wa watumishi wengi Askofu Moses Kulola |
Mchungaji Dunstan Maboya ambaye pia aliwahi kufanya kazi na Askofu Moses Kulola miaka ya nyuma hapa akielezea jambo |
Add caption |
RPC wa mkoa wa Mwanza Ernest Mangu akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Askofu Moses Kulola |
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mh Antony Dialo |
Mchungaji wa kanisa la EAGT Nkuhungu kaskazini mkoani Dodoma akiwa na baadhi ya wadau,,mchungaji huyu anafahamika sana mjini dodoma kwa kufanana na mheshimiwa waziri mkuu Mizengo Pinda |
Mchungaji Kadani Limbu ambaye ni Katibu wa Kanisa la EAGT Makao Makuu (Ujenzi) akisoma wasifu wa marehemu Askofu Kulola aliyezaliwa 1928 katika Kijiji cha Nyang’honge Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza na kujaliwa kupata elimu ya msingi (Middle School) na sekondari ya Bwiru Boys Mwanza kati ya mwaka 1946 hadi 1949 kuendelea na masomo na kupata Civil Technician.
Baada ya kumaliza na kupata utaalamu huo na kuajiliwa kuwa mtumishi wa serikali katika Halmashauri ya Mji wa Mwanza kama Mhandisi wa Mchoraji wa Ramani za majengo na Barabara wakati wa uhai wake aliamua kuacha kazi na kuanza utumishi wa mungu akifanya kazi kwa kutembea kila mahali akihubiri Injili kwa watu mbalimbali.
Wasifu huo ulimwelezea Askofu Kulola wakati wa utumishi wake wa kiroho alikuwa akitembea kwa miguu kuanzia mwaka 1962 baada ya kuacha kazi za serikali mwaka 1951 alipatwa na matatizo na kuwahi kufungwa gerezani na kupigwa na bwana jela na kuumizwa vibaya muguu wake wa kushoto na kupelekea kupata kilema na kuwekewa mguu wa bandia.
Marehemu Askofu Kulola ameacha mke na watoto 10 wajukuu 42 vitukuu 16 na amekuwa mutumishi wa kiroho kwa kuanzia akiwa na umri wa miaka 18 na jana amezihilisha kutokana na umati mkubwa uliofika kumuaga kwenye uwanja wa michezo wa kirumba Jijini Mwanza.