Katika hali isiyokua ya kawaida mgogoro ambao umekua gumzo nchini Tanzania unaohusisha masuala ya imani za kidini umechukua sura mpya baada ya mgogoro huo kuhamia hadi bungeni ambapo wabunge wamekua wakitupiana maneno yenye kushutumiana kuhusu nani ndie mhusika wa tatizo hili la udini kuzidi kukua kwa kasi nchini tanzania hususan masuala ya uchinjaji wa nyama,na masuala ya chama flani ni cha dini flan
Katika moja ya Hoja zilizozua utata ni pale mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Mh.Godbless Lema alipomtuhumu Rais Jakaya Kikwete kua muasisi wa tatizo la udini nchini Tanzania kauli iliyosababisha Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh,Job Ndugai kumpa wiki moja Mh.Lema kuthibitisha kauli hiyo ndani ya bunge.
wakati huohuo Mh.Ismail Aden Rage aliibuka na kupinga kauli hiyo kwa kutoa maelezo kua Rais Kikwete amekua muungwana katika suala hilo la udini kwani amekuwa wa kwanza kulikemea na kulitolea ufafanuzi wa kutosha na kuwataka viongozi wa dini zote kukutana na kujadiliana namna ya kudumisha amani ya nchi
katika kuonesha msisitizo hata katika muundo wa serikali yake katika mikoa .wakuu wa mikoa kutoka tanzania bara wakuu wa mikoa ambao ni wakristo wapo 19 huku wakuu wa mikoa ambao ni waislam wapo 9 kadhalika katika baraza la mawaziri na hata katika makatibu wa wizara mbali mbali idadi yake imewekwa kwa ulinganifu sawia alisema Rage
Katika kuendelea mjadala huo mbunge wa jimbo la Iramba magaribi Mh Mwigulu Nchemba aliibuka na kuutuhumu uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kudai kua katibu wa chama hicho Dr.Wilbroad Slaa nae alichangia katika kulikuza tatizo hilo ambapo katika mikutano aliyokua akiifanya mkoani singida alikua akikutana na viongozi wa dini ya kikristo na kugeuza mikutano hiyo kua ndio mikutano ya chama
Mwigulu Nchemba...alisema kwamba udini ni jambo geni hapa nchini,Tanzania imeongozwa na CCM tangu uhuru, na marais wote wamekuwa wakitoka ccm, rais wa kwanza alikuwa mkristo, wa pili muislam, wa tatu mkristo na wa nne ni muislam..akasema kama udini ni jambo geni watanzania tujiulize limekujaje???? Kwanini sasa na sio wakati huo???
kauli hii ilisababisha Mnadhimu toka kambi ya upinzani mh Tindu Lisu kusimama na kutaka Muongozo toka kwa Mh Naibu Spika Job ndugai hali iliyosababisha Naibu Spika kumlazimisha Mbunge huyo Lisu akae chini huku Lisu akikataa kwa kudai hakuna alichokosea hapo wakat ubishani huo ukiendelea ndipo Naibu Spika alipoita Askari wa bunge ili amtoe nje ya ukumbi wa Bunge Mh Lisu
"Askari toa huyu mtu njeeeeee nimesemaaa....we mtu gani kila saa unasimama wewe tuu tangu tumeanza umeshasimama zaidi ya mara 20" alisema Naibu Spika Mh.Job Ndugai
lakini kauli hiyo ilionekana kutofua dafu kwa mbunge huyo ambapo aligoma kutoka huku akipata sapot toka kwa wabunge wengine waliosikika wakitoa maneno
"hakuna kutokaa....huo ni uonevu....huo ubabe sasa""""
ubishani huo ulishababisha kikao hicho cha bunge kuvunjika hadi kufikia hatua ya "siwa" kifaa maalum ambacho huashiria kuendelea kwa shughuli za bunge kuingiziwa ndani na kikao hicho kuahirishwa hadi kesho asubuhi.
Wakati haya yakiendelea Rais Mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania Mh.Ally Hassan Mwinyi amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia masuala yanayoumiza vichwa wengi hususana tatizo hilo la udini husuan kwenye masuala ya uchinjaji na na kusema kua kila mtu afuate kile anachokiamini bila kuingilia uhuru wa mwingine,iwe ni katika kuchinja wanyama au popote pale
Katika moja ya Hoja zilizozua utata ni pale mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Mh.Godbless Lema alipomtuhumu Rais Jakaya Kikwete kua muasisi wa tatizo la udini nchini Tanzania kauli iliyosababisha Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh,Job Ndugai kumpa wiki moja Mh.Lema kuthibitisha kauli hiyo ndani ya bunge.
Mh.Godbless Lema |
Mh.Ismail Aden Rage |
katika kuonesha msisitizo hata katika muundo wa serikali yake katika mikoa .wakuu wa mikoa kutoka tanzania bara wakuu wa mikoa ambao ni wakristo wapo 19 huku wakuu wa mikoa ambao ni waislam wapo 9 kadhalika katika baraza la mawaziri na hata katika makatibu wa wizara mbali mbali idadi yake imewekwa kwa ulinganifu sawia alisema Rage
Katika kuendelea mjadala huo mbunge wa jimbo la Iramba magaribi Mh Mwigulu Nchemba aliibuka na kuutuhumu uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kudai kua katibu wa chama hicho Dr.Wilbroad Slaa nae alichangia katika kulikuza tatizo hilo ambapo katika mikutano aliyokua akiifanya mkoani singida alikua akikutana na viongozi wa dini ya kikristo na kugeuza mikutano hiyo kua ndio mikutano ya chama
Mwigulu Nchemba...alisema kwamba udini ni jambo geni hapa nchini,Tanzania imeongozwa na CCM tangu uhuru, na marais wote wamekuwa wakitoka ccm, rais wa kwanza alikuwa mkristo, wa pili muislam, wa tatu mkristo na wa nne ni muislam..akasema kama udini ni jambo geni watanzania tujiulize limekujaje???? Kwanini sasa na sio wakati huo???
Mh Mwigulu Nchemba |
"Askari toa huyu mtu njeeeeee nimesemaaa....we mtu gani kila saa unasimama wewe tuu tangu tumeanza umeshasimama zaidi ya mara 20" alisema Naibu Spika Mh.Job Ndugai
Naibu Spika Mh.Job Ndugai |